Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchungaji Senny amchana Geordavie kuchorwa tattoo 'ni ukahaba'

Geordavie Tattoo Senny Mchungaji Senny amchana Geordavie kuchorwa tattoo 'ni ukahaba'

Mon, 5 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiongozi wa Makanisa ya Infinity jijini Arusha, Mchungaji Joel Senny ameamua kuvunja ukimya na kuponda kitendo cha kiongozi mwenzake wa kiroho wa Ministry ya Ngurumo ya Upako, Nabii Mkuu Geordavie ambaye ali-trend hivi karibuni baada ya kuchorwa tattoo na mwanamke.

Haya ayamejiri baada ya wanahabari kuhoji kuhusu baadhi ya wachungaji kudaiwa kusababisha kuvunjika kwa ndoa za watu huku wanamama Elizabeth akidai pia kuwa mume wake amemkimbia kwa sababu ya kujichora tatoo ya Nabii huyo lakini baadaye alikana kuvunjika kwa ndoa yake.

"Suala la viongozi wa dini kuvunja ndoa za watu linatokana na watu kutojitambua, na mahubiri kuzagaa ambayo sio ya Kibiblia.

“Kuna watu wanaogopa kuzungumzia hili lakini sio mimi, sitamsema mtu vibaya lakini ukija kwenye jamii, basi tutakujibu kwenye jamii. Kwa mfano mtu kujichora tattoo, kama ulikuwa na ujasiri wa kutuonyesha hiyo tattoo na tukaiona maana yake ulikuwa unatafuta ulichokitafuta na utakipata.

“Mchungaji anasema huyu mwanamke ana mahaba na yeye, mahaba ni nini….? Ni driving force ya kuendea kwenye ukahaba, kwa hiyo alichokuwa akikionyesha pale ni ukahaba tu wa kawaida.

“Pesa watu wanazozitoa zinaliwa, zinagawiwa… hapana, sisi viongozi wa dini tuna mambo mengi, kama chanzo cha pesa halali kinajulikana kwa mba ni sadaka, kwa Arusha hii labda mtumishi wa Mungu ana vyanzo vingine vya mapato, siwezi kumsemea sana.

“Lakini kwa sadaka hiyo ya watu wanaonenda pale ya buku buku na buku jero, huwezi kugawa sadaka namna ile, hata mimi siwezi kukupa hela bila kuifanyia kazi labda mkamhoji yeye vyanzo vyake vya mapato ni vipi.

“Kwa hivi tuna waharibu waumini wala huo sio moyo wa utoaji. Kama ingekuwa ni moyo wa utoaji wangepewa wote, lakini wanaopewa ni mpaka wamsifie, tattoo peke yake ilivuna milioni saba, mimi natamani nijipige kabisa picha sijui nitavuna milioni 100?” amesema mchungaji Joel.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live