Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchungaji Msigwa kumfikisha RC Hapi mahakamani

20510 MSIGWA TanzaniaWeb

Wed, 3 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Iringa. Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa ameingia katika ‘vita’ na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi akibainisha kuwa atamfikisha mahakamani kufuatia uamuzi wake wa kumuweka ndani diwani wa Viti maalum wa chama hicho kikuu cha upinzani nchini, Silestina Jonso.

Leo Oktoba 2, 2018, Msigwa akizungumza na waandishi wa habari mjini Iringa amesema Hapi alimdhalilisha diwani huyo.

“Alidiriki kumdhalilisha diwani wetu, sheria iko wazi sana, vipengele vyote vile mkuu wa mkoa hakufuata, amekiuka, ametoa amri ya kumpeleka diwani wetu polisi kinyume cha sheria,” amesema.

“Sasa kwa sababu amekiuka taratibu, mimi kama mwenyekiti wa kanda na mbunge ili kukomesha tabia hii ya RC Hapi  tumwambie hatukubaliani naye na hatujalala, anakuja na sheria zake za kutisha watu na kuwatia ndani.”

Ameongeza, “tumejipanga vizuri tunamfungulia kesi mahakamani kwa sababu anatumia madaraka yake vibaya. Tutakutana naye mahakamani kwa sababu anatumia madaraka vibaya.”

Amemtaka Hapi kufanya kazi  kwa kuzingatia mamlaka yake, “Mimi ni mbunge halali wa wananchi natimiza majukumu yangu.”

Hivi karibuni Hapi aliagiza kuwekwa ndani kwa diwani huyo kutokana na kuibuka kwa mgogoro wa nyumba mkoani humo.

Chanzo: mwananchi.co.tz