Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchina afikishwa kortini kwa kumpa kipigo Mtanzania

Supreme Court Sets Out Object And Purpose Of Order VII Rule 11 Of The Code Of Civil Procedure1908.pn Mchina afikishwa kortini kwa kumpa kipigo Mtanzania

Sun, 26 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi limesema Raia wa China, Zheng Yuan Feng ambaye ni Mfanyakazi wa Kampuni ya CRCC upande wa jikoni katika mradi wa SGR kambi ya Fela, amefikishwa Mahakamani juzi Machi 24, 2023 kwa kosa la kumjeruhi Mfanyakazi mwenzie (Mwanamke) Mtanzania wakiwa eneo la kazi katika kambi hiyo.

Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime, imesema “Katika mitandao ya kijamii ikiwepo makundi binafsi, kumeonekana taarifa inayosambazwa ikieleza kuwa kuna Mfanyakazi mmoja (Dada) Mtanzania katika mradi wa SGR kambi ya FELA amejeruhiwa na Mfanyakazi wenzake upande wa jikoni Raia wa China wote wakiwa ni Wafanyakazi wa kampuni ya CRCC”

“Jeshi la Polisi lingependa kueleza kuwa tukio hilo ni kweli liliripotiwa Polisi na ushahidi ulikusanywa na Mtuhumiwa huyu ZHENG YUAN FENG alifikishwa Mahakamani March 24,2023.

Picha za Mwanamke huyo zilizosambaa kwenye Mitandao ya kijamii zimemuonesha akiwa amelala sakafuni huku akitokwa damu nyingi usoni kuliko na jeraha alilosababishiwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live