Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbwa wamegeuka kero Mbozi

Mbwa Koko Iringa Mbwa wamegeuka kero Mbozi

Fri, 8 Sep 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Baadhi ya wakazi wa mji wa Vwawa, wilayani Mbozi; mkoa wa Songwe, wamedai wanaishi kwa hofu kufuatia kundi la mbwa linalozurura mtaani nyakati za mchana.

Wamesema hayo leo Ijumaa September 9, 2023 walipozungumza kwa nyakati tofauti na Mwananchi Digital, kwamba baadhi ya wafugaji wameshindwa kuwadhibiti mbwa wao na kuacha wakizurura hovyo mtaani na kutishia usalama wa watu.

Mkazi wa Vwawa mjini Helbert Kayuni amesema kumekuwepo na tabia ya wafugaji wa mbwa kuwaachia wakizurura hovyo mtaani, ambapo baadhi ya mbwa wanakamata kuku, huku wengine wakitishia usalama wa watu na hasa watoto.

"Kuna wakati ambapo mbwa hao walikuwa kuwashambulia watoto na mmoja walimjeruhi vibaya sana kiasi ikalazimika kwenda kutibiwa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Nyanda za juu Kusini Mbeya," amesema Kayuni.

Naye Monika Mbwile amesema Mbwa wanaozurura mtaani wanawatishia na kusababisha hofu, na kuwa mamlaka husika zichukue tahadhari ikiwezekana kuwaua mbwa hao ama kuwachukilia hatua wamiliki.

"Miaka ya nyuma lilikuwepo zoezi la kuwapiga risasi mbwa wote wanaozurura, hali hiyo ilisaidia kuondoa kero hiyo mtaani," amesema Mbwile.

Kwa upande wake Ofisa Mifugo Wilaya ya Mbozi, Isack Mahai; ametoa wito kwa wafugaji kufuga mbwa kwa kufuata sheria ikiwa ni pamoja na kuwapatia chanjo, ili kujilinda na madhara ya ugonjwa wa kichaa cha mbwa.

Amesema chanjo inawazuia mbwa hao wasipate ugonjwa wa kichaa cha mbwa hata waking’atwa na mbwa mwitu ambapo ameeleza dalili za mbwa mwenye ugonjwa wa kichaa kuwa ni kutoa mate mengi na kung’ata ng’ata vitu hovyo wakiwamo binadamu na hata miti.

Aidha amewataka wananchi kuzingatia vibali vya kumiliki na kuchanja mbwa ili kuepuka faini ya Sh10 milioni kwa anaekiuka sheria hiyo.

Pia Mahai amesema wamiliki wa mbwa wanapaswa kuwatumia mbwa kwa ulinzi wa usiku, lakini mchana wafungiwe ndani kwa mnyororo.

Chanzo: Mwanaspoti