Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbwa aua watu wawili Geita

Mbwa Wachomwa Moto Hadi Kufa Afrika Kusini Baada Ya Kumshambulia Mtoto Mbwa aua watu wawili Geita

Fri, 9 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu wawili wamefariki Mkoani Geita kwa kung’atwa na mbwa anaeyedhaniwa kuwa ni kichaa huku wengine wanne wakiendelea kupata matibabu katika Hospitali zilizopo katika Mkoa huo.

Ezekiel Emmanuely ni Baba wa Hosea Ezekiel (20) ambaye amefariki kwa kung’atwa na mbwa huyo na amesema Mwanae aling’atwa wakati akielekea Kanisani.

Baadhi ya Wananchi wameiomba Serikali kufanya jitihada na kuchukua hatua stahiki katika kuwapa chanjo mbwa hao wanaoishi katika Mitaa mbalimbali ya Geita.

Kaimu Mganga Mfawidhi Kituo cha Afya cha Katoro Dkt.Zacharia Shija amekiri kuwepo kwa vifo hivyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live