Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge alia uhaba vyumba vya kuhifadhia maiti

Maiti Mbunge alia uhaba vyumba vya kuhifadhia maiti

Thu, 18 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki, Hamis Taletale ameipongeza Serikali kwa kazi nzuri ya kuboresha Sekta ya Afya Jimboni kwake ikiwemo kupeleka Ambulance Kituo cha Afya Mkuyuni lakini hata hivyo amesema Jimbo hilo halina chumba cha kuhifadhia maiti hivyo kupelekea Mtu anapofariki maiti kwenda kuhifadhiwa Morogoro Mjini.

Akiongea Bungeni Jijini Dodoma wakati akichangia Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Rais TAMISEMI, Tale amesema;

“Tunamshukuru Mh. Rais kwa kutuletea Vituo vya Afya lakini hatuna sehemu ya kuhifadhia maiti leo hii tukipata maiti Morogoro Kusini Mashariki lazima tukahifadhi Morogoro Mjini sasa samahani kwa kusema hivi Mtu anaona Mtu ana rest in peace lakini hapa ana-rest na stress, Mtu umefiwa halafu bado utafute gari ya kwenda kuhifadhi maiti Mjini”

“Mh. Mchengerwa tunakuomba ufike Morogoro Kusini uone changamoto zetu”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live