Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge Tarimo ataja elimu kusaidia maendeleo ya jamii

Shule Pic Mbunge Tarimo ataja elimu kusaidia maendeleo ya jamii

Sun, 9 Jul 2023 Chanzo: Mwananchi

Mbunge wa Moshi Mjini (CCM), Priscus Tarimo, ameupongeza uongozi wa Shule ya Sekondari ya St Maria Goreti kwa mchango wa kukuza sekta ya elimu na mchango na kusaidia wananchi masuala ya kijamii.

Tarimo alitoa pongezi hizo juzi Julai 7, 2023 wakati wa kambi maalumu ya kupima afya na kuchangia damu iliyoandaliwa na uongozi wa shule hiyo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya kuelekea miaka 25 tangu kuanzishwa kwa shule hiyo.

“Shule hii ilianza kama ya sekondari ya kawaida, baadaye ikawa ya hadi kidato cha sita; sasa hivi uongozi wa shule hii umeanzisha shule ya awali na ya msingi, haya ni mafanikio makubwa kwa shule yenu na mchango mkubwa katika kukuza sekta ya elimu hapa nchini," alisema Tarimo.

Pia, aliupongeza uongozi wa shule hiyo kwa kuchangia maboresho ya mazingira mkoani Kilimanjaro kwa kutoa miche ya miti na uaandaji wa miti katika wilaya zote za mkoa.

“Nimeelezwa ya kuwa mmechangia miti 2,000 itakayopandwa maeneo mbalimbali hapa mkoani Kilimanjaro, huu ni mchango mkubwa katika kuboresha mazingira hasa ikitiliwa maanani ya kuwa moja wapo ya ajenda za Serikali ni kuhakikisha mazingira yanaboreshwa ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi," alisema.

Kuhusu kambi hiyo, Tarimo wananchi walipata fursa ya kuchangia damu ili kuokoa maisha ya wananchi wengine sambamba na kupima hali zao za afya bure.

Tarimo ambaye katika hafla hiyo alijisajili kama mshiriki wa mbio zilizoandaliwa katika maadhimisho hayo, pia aliupongeza uongozi wa shule hiyo kwa kuandaa mbio hizo zinazochangia kuboresha maisha ya washiriki sambamba na kukuza sekta ya michezo.

Awali, akimkaribisha mbunge huyo kutoa salamu zake, Mkuu wa St Maria Goreti Clementina Kachweka, alisema kambi hiyo imeandaliwa kwa ajili ya kuchangia damu kwa wahitaji kwa kuwa mahitaji yamekuwa makubwa katika taasisi za tiba mkoani Kilimanjaro.

“Mbali na kuchangia damu, pia watu wanapata fursa za kupima afya zao bure, lengo ni kuwapa watu kuweza kujua hali zao za kiafya na pale anapogundulika kuwa na maradhi aweze kuanza tiba mapema,” alisema.

Aliishukuru Hospitali ya KCMC ya Moshi kwa kuwa mstari wa mbele katika kuratibu zoezi hilo la upimaji afya na kuchangia damu huku wakisaidiwa na wataalamu wengine kutoka Hospitali ya St Joseph, Hospitali ya Huruma na Masispaa ya Moshi (kitengo cha Damu Salama).

Zaidi ya watu 1000 wakiwamo wanafunzi walipima afya na kupata ushauri mbalimbali huku watu 50 wakichangia damu itakayookoa maisha ya watu 150.

Clementina alisema mbali na huduma hiyo, pia uongozi wa shule hiyo umeshafanya matukio mengine ikiwamo uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 25 tangu kuanzishwa kwa shule hiyo na ugawaji wa miti 2,000 kwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro itakayopandwa maeneo mbalimbali mkoani humo.

“Mbali na shughuli hizo, pia zitafuata shughuli zingine ambazo ni mbio, matembezi ya hisani km 10 na km 5 zitakazofanyika Agosti 26, 2023 na ambazo usajili wake umeanza leo, (Julai 7),” alisema

Chanzo: Mwananchi