Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbunge CCM azungumzia kifo cha mfanyabiashara wa Arusha

Wed, 22 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Mbunge wa Arumeru Mashariki (CCM), Dk John Pallangyo amesema kifo cha mfanyabiashara maarufu wa madini, Thomas Mollel maarufu kama Askofu kimemsikitisha na kumuumiza.

Akizungumza na Mwananchi katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma leo Jumatano Mei 22, 2019 mara baada ya kumaliza kuapishwa kuwa mbunge, Dk Pallangyo amesema, “Ni tukio ambalo limetuumiza sana.”

Amesema Askofu alikuwa mtu wake wa karibu ambaye licha ya kuwa mgonjwa alihakikisha anasafiri kutoka Arusha kwenda Dodoma kushuhudia tukio la kuapishwa kwake kuwa mbunge kuchukua nafasi ya Joshua Nassari wa Chadema aliyepoteza sifa za kuwa mbunge.

Dk Pallangyo amesema waliagana na mfanyabishara huyo maarufu na kuahidi kuwa watakutana Dodoma lakini hali imekuwa tofauti kwani alipofika Dodoma wamekutana wakati Askofu akiwa hawezi kuongea tena.

Amesema alipofika Dodoma Askofu alikwenda kushiriki chakula na wenzake na baada ya hapo alipigiwa simu kuwa mfanyabashara huyo alidondoka na baadaye kupelekwa hospitalini ambako baadaye kidogo akapigiwa simu kuwa amefariki dunia.

Kuhusu taratibu za kuusafirisha mwili, amesema utasafirishwa Jumapili ya Mei 25, 2019 kwa Ndege ya Shirika la ATCL kupitia Dar es Salaam na taratibu za mazishi zinaendelea jijini Arusha.

Pia Soma

Chanzo: mwananchi.co.tz