Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbozi walia na maji, sehemu ya kutupa taka

64913 Pic+mbozi

Tue, 2 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mbozi.  Wafanyabiashara wa eneo ambalo maonyesho ya kimondo hufanyika wamesema kuna changamoto ya ukosefu wa maji na miundombinu ya kutupa taka katika eneo hilo ambalo wakati wa maonyesho linakuwa na wageni wengi.

Maonyesho hayo yanafanyika katika eneo la Ndolezi kilipo kimondo cha Mbozi mkoani Songwe, yalizinduliwa Juni 28. Tangu siku hiyo kumekuwa na shughuli mbalimbali kama mashindano ya mbio za baiskeli, ngoma za asili na upishi wa vyakula vya asili hali iliyofanya eneo kuchangamka wakati wote.

Wakizungumza na MCL Digital leo Juni 30 (siku ya kilele cha maadhimisho hayo), wanasema tangu maadhimisho hayo yalipozinduliwa kumekuwa na wageni wengi ambao wamekuwa na matokeo chanya katika biashara zao lakini mazingira yana changamoto

Mmoja wa wafanyabiashara wa eneo hilo Neema Nwashiuya amesema anakabiliana na changamoto ya ukosefu wa huduma ya maji katika biashara yake ya mgahawa, lita 20 za maji anazinunua kwa Sh1,000.

Mwingine ni Christina Msongole ambaye amesema changamoto nyingine ni kukosekana kwa maelekezo au eneo maalumu la kutupa taka hivyo baadhi ya watu kuzitupa hovyo jambo ambalo ni hatari kwa afya za watu.

Hata hivyo licha ya Changamoto hizo Mkuu wa mkoa wa Songwe Brigedia Jenerali ( mstaafu) Nicodemus Mwangela amewatangazia wananchi kuwa kutakuwa na siku saba za ziada kuendelea na biashara katika eneo baada ya siku ya kilele (leo).

Pia Soma

Chanzo: mwananchi.co.tz