Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbowe aikumbuka UKAWA

Mbowe Db Mbowe aikumbuka UKAWA

Wed, 25 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amesema ushindi wa vyama vya upinzani katika Uchaguzi Mkuu wa 2015, ulitokana na ushirikiano wao kupitia mwamvuli wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), uliwasaidia wapinzani kupata viti vingi vya ubunge na udiwani. 

Mbowe ametoa kauli hiyo leo tarehe 24 Oktoba 2023, akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Jimbo la Nkasi Kaskazini, mkoani Rukwa, wakati akizungumzia chaguzi zijazo.

“Ukawa ilijumuisha Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD, tukapewa na wengine kutoka CCM tukatengeneza jeshi kubwa la kisiasa tukaingia uchaguzi wa 2015. Naomba niwatangazie tuliweza kuzoa viti vya ubunge na udiwani na mgombe a wetu akashinda kura za urais lakini wenzetu hakukubali vyama vingine vina haki ya kushika madaraka ya nchi,” amesema Mbowe.

Mbowe amesema “Chadema na washirika wetu tulishinda viti vya ubunge 146 ambayo vilitosha kuunda serikali, wakavichakachua wakatuachia 115 ambavyo havikutuwezesha kuendesha Serikali. Tulishinda kuongoza majiji makubwa katika nchi hii.”

Akizungumzia chaguzi zijazo, Mbowe amewataka wananchi waichague Chadema, akidai ni chama cha haki “tunapokwenda kwenye chaguzi zinazofuata lazima wewe mwananchi uamue unafungamana na upande gani, upande wa giza au upande wa mwanga na haki utasimama na Chadema.”

Katika hatua nyingine, Mbowe ameitaka Serikali ipeleke bungeni muswada wa marekebisho ya katiba, yatakayowezesha upatikanaji wa tume huru ya uchaguzi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live