Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbeya kudhibiti wahamiaji haramu

UHAMIJI HARAMU.jpeg Uhamiaji Mbeya waweka mkakati kudhibiti wahamiaji haramu

Sat, 23 Oct 2021 Chanzo: mwananchidigital

Kufuatia tukio la kukamatwa kwa dereva wa loru, Enock Moses (40) aliyekuwa akisafirisha wahamiaji haramu 12 kutoka Chalinze Mkoa wa Pwani kwenda Mkoa wa Mbeya, Idara ya Uhamiaji mkoani humo imeweka mikakati ya kufuatilia wa mtandao wa watu wanaowaingiza wahamiaji hao nchini.

Ofisa uhamiaji Mkoa wa Mbeya Kamishana Msaidizi wa uhamiaji, Kigongo Shikille ameliambia Mwananchi jana Ijumaa Oktoba 22, 2021 kuwa mbali na kuendelea kumshikilia dereva huyo kwa uchunguzi, wanaendelea kuimarisha doria katika mipaka ya Malawi na Zambia.

"Juzi Oktoba 19, 2021, askari wetu wakiwa katika doria katika kituo cha ukaguzi Inyala wamelikamata lori lililokuwa limebaba shehena ya vifaa vya ujenzi likitokea jijini Dar es Salaam likiwa limewaficha wahamiaji haramu 12 raia wa Ethiopia ambao alitakiwa kuwashusha Uyole jijini hapa ili wasafirishwe kwenda nchini Afrika Kusini," amesema.

Amesema kuwa mbali na kufuatilia mtandao huo pia wataimarisha ulinzi na doria katika maeneo ya mikoa inayopakana na nchi jirani za Malawi na Zambia ambako inadhaniwa ndio njia zao kuu na kuna watu ambao wanawaongoza na kufanikisha kuwavusha," amesema.

Shille amesema kuwa kutokana na biashara ya kusafiriaha wahamiaji haramu nchini kuwa katika mnyororo wa watu wengi kwa kuwatumia madereva, kwa sasa biashara hiyo itadhibitiwa kikamilifu.

"Kimsingi madereva ni chambo, ila wapo ambao ndio wahusika wakubwa wako kwenye mnyororo wa kuvusha wahamiaji haramu kutoka mataifa mbalimbali umefika wakati kuachana na tabia hiyo kwa madai kuwa vyombo vya ulinzi na usalama havijalala," amesema.

Mkazi wa Jijini Mbeya, Salome Isack ameshauri vyombo vya Dola kushirikiana na wenyeviti wa Serikali ya Mitaa na wajumbe wa nyumba 10 kufanya doria nyumba kwa nyumba kwani wapo wahamiaji haramu ambao tunaishi nao katika jamii na wanafumbiwa macho.

Chanzo: mwananchidigital