Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbaroni kwa kukata nguzo ya umeme kwa shoka

Nguzo Hy.jpeg Mbaroni kwa kukata nguzo ya umeme kwa shoka

Mon, 10 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Serikali ikiendelea na mpango wake wa kueneza nishati ya umeme vijijini huko Kijiji cha Nkiniziwa wilayani Nzega mkoani Tabora, mtu mmoja amekamatwa kwa tuhuma za kukata kwa shoka nguzo ya umeme na kuacha nyaya zikining’inia na kusababisha baadhi ya vijiji jirani kukosa huduma ya umeme.

Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mtu huyo aliyekata nguzo hiyo anadaiwa kuwa ni mhalifu na kwamba hii ni nguzo ya pili na kwamba katika kutekeleza tukio hilo alipigwa na shoti na kunusurika kifo na kwasasa mtuhumiwa amelazwa katika Kituo cha Afya Busondo wilayani Nzega.

TANESCO bado wanafuatilia tukio hilo na kwa mujibu wa taarifa za awali mtuhumiwa huyo amekata nguzo inayosafirisha umeme mkubwa wa Kilovolt 132.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live