Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (TANGA UWASA) kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi limefanikiwa kumdaka mwizi wa maji katika eneo la Donge (Maarufu kama kwa Mama Sigara) ambae alikuwa amejiunganishia huduma ya Maji kinyume na utaratibu ambapo baada ya kubainika huduma imesitishwa katika eneo hilo mpaka pale taratibu za kisheria zitakapo kamilika.
Akizungumza katika tukio hilo Mwenyekiti wa Mtaa huo Ndugu Saidi Rajabu amesema kuwa mtuhumiwa ni kijana anaeishi peke yake katika makazi hayo na alipopata tetesi za uwepo wa tabia hiyo alianza mara moja jitihada za kufanya uchunguzi kwa kushirikiana na mafundi wa TANGA UWASA ili kubaini uhalisia ndipo wakafinikiwa kumkamata.
Kwa Upande wa TANGA UWASA limeendelea kuwasisitiza wananchi kutoa taarifa za uwepo wa matukio ya wizi wa maji ili kuzuia upotevu wa maji ambapo wamesema donge nono itolewa kwa taarifa zote zitakazothibitishwa.