Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbarawa azindua mradi wa Bilioni 1.7/- Mpanda

Sekta Ya Usafirishaji Inahitaji Wataalamu Wa Kutosha   Prof Mbarawa.jpeg Mbarawa azindua mradi wa Bilioni 1.7/- Mpanda

Mon, 28 Oct 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa ameweka mawe ya msingi na kuzindua miradi minne ya maendeleo yenye jumla ya shilingi bilioni 1.7 katika Manispaa ya Mpanda, mkoani Katavi.

Katika siku ya pili ya ziara yake mkoani humo, Oktoba 27, 2024, Waziri Mbarawa amefanya ukaguzi wa ukarabati wa Hospitali ya Manispaa ya Mpanda ambao umegharimu kiasi cha shilingi milioni 900, pamoja na kuweka jiwe la msingi kwa ujenzi wa shule mpya ya msingi ya Kawajense ambayo ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 100 kwa gharama ya shilingi milioni 561.

Pia ameweka jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vitano vya madarasa na matundu sita ya vyoo katika Shule ya Sekondari Magamba, ambao umegharimu shilingi milioni 144.

Aidha, amekagua na kuweka jiwe la msingi kwenye mradi wa ukarabati wa vyumba sita vya madarasa, ofisi moja ya walimu, na matundu tisa ya vyoo katika Shule ya Msingi Kashaulili uliogharimu shilingi milioni 188.

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika eneo la Kazima Ringini, Manispaa ya Mpanda, Waziri Mbarawa amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayofanya na kutoa wito kwa wananchi kuitunza miundombinu hiyo ili iweze kudumu na kunufaisha vizazi vijavyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live