Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbarawa akerwa na watumishi watatu Newala aagiza warejeshwe utumishi

62952 Pic+mbarawa

Sun, 16 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Newala. Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa ameagiza kuondolewa kwa watumishi watatu wa mamlaka ya maji ya Makonde wilayani Newala kwa tuhuma za kuvuruga mamlaka hiyo na kusababisha wananchi kuendelea kukabiliwa na kero ya maji.

Watumishi hao ni pamoja na Julius Jongolo (Mhasibu), Denis Ngowi na Lista Katalabalo (wahandisi).

Profesa Mbarawa ametoa agizo hilo leo Jumapili Juni 16, 2019 alipokuwa akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Namiyonga.

Amesema baadhi ya watumishi hao si waadilifu, wamekuwa wakifanya hujuma hata kwenye ukusanyaji wa mapato.

“Watendaji watatu kwa asilimia kubwa wanavuruga mamlaka na mpaka leo wizara hatujafanya maamuzi inasikitisha sana, wenzetu wanafanya kazi lakini wizara tunawarudisha nyuma, Jumatatu (kesho)  hawa tutahakikisha tumewaondoa na kuwarudisha utumishi,” amesema Mbarawa.

Aidha ameagiza kutenganishwa kwa mita za umeme katika mamlaka ya maji Makonde na nyumba za wafanyakazi na kila mmoja awajibike na bill (ankara) yake.

Pia Soma

Awali, Mkuu wa Wilaya ya Newala, Aziza Mangosongo amesema kutokana na  mamlaka hiyo pamoja na wafanyakazi kutumia mita moja kumesababisha mamlaka hiyo kuwa na deni kubwa lakini pia kutokuwa na nidhamu ya matumizi ya umeme kwa wafanyakazi.

Chanzo: mwananchi.co.tz