Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbarawa aanza na upatikanaji wa maji kwa wateja D’Salaam

10764 Mbarawa+pic TanzaniaWeb

Thu, 5 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa ameiagiza Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (Dawasco) kuwaunganishia maji wateja 850,000 ifikapo mwisho wa mwaka huu wa fedha.

Profesa Mbarawa alisema hajaridhishwa na idadi ndogo ya wateja 290,000 ambayo Dawasco imefikisha, akidai watu wengi wanahitaji maji lakini hawajafikiwa na mamlaka hiyo.

Akizungumza na wafanyakazi wa Dawasco Dar es Salaam jana, ikiwa ni siku mbili baada ya kuteuliwa kuwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Mbarawa aliwataka Dawasco kuongeza kasi ya kuwaunganishia maji wananchi ili nao waongeze mapato yao yatokanayo na mauzo ya maji.

Waziri huyo alieleza kusikitishwa na upotevu mkubwa wa maji ambao ni zaidi ya asilimia 40 ya maji yote yanayozalishwa Dar es Salaam ambayo ni lita za ujazo 502,000 kwa siku. Alisema kiasi hicho ni kikubwa na kinaisababishia mamlaka hiyo hasara.

“Kule mitaani kuna upotevu mkubwa wa maji, nataka mwende huko. Kila nikipita mtaani kwangu nakuta maji yanavuja na hakuna anayejali, wananchi wanawaona hamko serious, jipangeni kudhibiti upotevu wa maji,” alisema.

Awali akiwasilisha taarifa ya utendaji kazi wa mamlaka hiyo kwa Waziri Mbarawa, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco, Mhandisi Cyprian Luhemeja alisema mamlaka hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwamo upotevu wa maji.

Luhemeja alisema Dawasco inapoteza asilimia 44 ya maji yanayosambazwa kwa wananchi wa Dar es Salaam na maji hayo yanapotea kwa njia za kuvuja kwa mabomba mitaani na mita za maji kusoma kiasi kidogo cha matumizi ya maji kutokana na uchakavu wake.

Chanzo: mwananchi.co.tz