Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbarawa: Wakazi Bonyokwa kununua maji dumu Sh500 itakuwa historia

32037 PIC+MBARAWA Tanzania Web Photo

Mon, 17 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Changamoto ya uhaba wa maji katika Kata ya Bonyokwa jijini Dar es Salaam inatarajiwa kuwa historia baada Waziri wa Maji na Umwagiliaji,  Profesa Makame Mbarawa kuagiza maji kufika eneo hilo ndani ya wiki mbili kuanzia leo Jumatatu Desemba 17, 2018.

Amesema nia ya Serikali ni kuhakikisha maji yanawafikia wananchi katika maeneo yao, hasa yale yenye uhaba mkubwa wa maji.

Ametoa kauli hiyo leo alipotembelea kata hiyo na kukagua zoezi la uchimbaji wa mitaro kwa ajili ya kutandaza mabomba.

“Tunataka tatizo la maji Bonyokwa liwe historia maana nilipata taarifa kuwa wananunua dumu kwa Sh500, jambo hili halipaswi kuvumiliwa. Tunawaletea maji kazi kwenu kuyavuta,” amesema Profesa Mbarawa wakati akizungumza na wananchi wa eneo hilo.

Wakazi hao walishukuru kwa hatua hiyo kwa kile walichodai kuwa wameteseka kwa muda mrefu kutokana na ukosefu wa maji.

“Binafsi nimekuwa nikitumia Sh5000 hadi Sh7000 kwa siku kununua maji. Sasa hatua ya kutuletea maji inatupa faraja mno wakazi wa Bonyokwa,” amesema Sharifa Said, mkazi wa Bonyokwa.



Chanzo: mwananchi.co.tz