Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbarali wajipanga kukabili homa ya nguruwe

Nguruwe Pic Mbarali wajipanga kukabili homa ya nguruwe

Fri, 10 Feb 2023 Chanzo: Mwananchi

Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya imeanza kuchukua hatua za kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa homa ya nguruwe kwa kupiga marufuku usafirishaji wa mifugo kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

Hatua hiyo imekuja baada ya kuibuka kwa ugonjwa huo katika Mikoa ya Mbeya, Iringa Njombe na mji wa Makambako ambayo imepakana na Wilaya hiyo.

Mkuu wa Idara ya kilimo na Mifugo na Uvuvi Wilaya ya Mbarali, Dk Anania Sangwa ametoa taarifa hiyo leo Ijumaa Februari 10, 2023 kwenye kikao cha Baraza la Madiwani na kuwataka kuanza kuchukua tahadhari kutokana na kupakana na mikoa ambayo kuna milipuko wa homa ya nguruwe.

“Idara yetu imepata taarifa kuwa mikoa ya jirani ikiwepo Mbeya, Iringa na Njombe kumeibuka ugonjwa huo, hivyo sasa ni wakati wa kuchukua hatua za kudhibiti ikiwepo kupiga marufuku kusafirisha kutoka sehemu moja kwenda nyingine” amesema.

Amesema kufuatia uwepo wa ugonjwa huo jamii kufikishiwa taarifa na kupatiwa elimu ya kukinga mifugo ikiwepo usafirishaji, kuachia ikizurura ovyo mitaani na kufanya ukaguzi wa magari yanayosafirisha katika maeneo ya mipakani.

“Pia wafugaji waepukane na tabia ya kuokota mabaki ya mifupa ya nguruwe kwa ajili ya kulisha mifugo kwani kuna uwezekano mkubwa ikawa na virusi vya homa ya nguruwe na kusababisha kusambaa zaidi,” amesema.

Dk Sangwa ameongeza kuwa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya hiyo imeanza kudhibiti katika maeneo ya mipakani kwa ukaguzi wa magari na vibali vya usafirishaji kwa madereva wa magari makubwa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Mbarali, Twalib Lubandamo, amewataka wananchi hususan wafugaji kuchukua tahadhari ya matumizi ya nyama ya mifugo hiyo ili kuepuka kupata virusi vya homa ya nguruwe.

“Tunawataka wananchi kuchukua tahadhari na sio kupuuzia taarifa zinazotolewa na wataalam wa mifugo ikiwepo kula nyama ya nguruwe isiyoiva sana,” amesema.

Naye Katibu Tawala wilayani humo, Michael Semindu amesema tayari hatua zimeanza kuchukuliwa kwa kukabiliana na ugonjwa huo, ikiwepo kupiga marufuku usafirishaju wa nguruwe sambamba na kufanya ukaguzi wa mara kwa mara maeneo ya mipakani.

Mkazi wa Ubaruku Wilaya ya Mbarali, Mathias Shija amesema kuna kila sababu Serikali kutoa elimu kwa jamii ikiwepo mikusanyiko ya watu hususan kwenye vilabu vya pombe za kienyeji.

“Tuombe elimu itolewe kwenye vilabi vya pombe za kienyeji kwani ndio kuna ulaji holela wa nyama ikiwepo utumbo, miguu ambavyo sio salama sana kws matumizi ya binadamu,” amesema.

Chanzo: Mwananchi