Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mazoezi kikosi cha Zimamoto yazua taharuki Bukoba

69421 MOTO+PIC

Fri, 2 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Bukoba. Taharuki ilitanda leo Alhamisi  Agosti Mosi, 2019 wakati Jeshi la Polisi Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji kikifanya mazoezi ya kuzima moto katika uwanja wa ndege wa Bukoba.

Hali hiyo iliwafanya wananchi kuamini kuna ndege imeanguka, kuchochewa zaidi na magari ya kikosi hicho  yaliyokuwa yakielekea na kutoka katika uwanja huo, yakiwa yamepakia watu waliokuwa wakiigiza kama majeruhi waliokuwa wakipelekwa hospitali.

Evarista Mutasingwa wamesema aliamini ni tukio la kweli baada ya ulinzi mkali kuimarishwa na magari ya usalama kuongezeka.

Zoezi hilo lililoshirikisha vikosi mbalimbali halikujulikana na limetajwa kama hatua ya kupima utayari iwapo litatokea tatizo linalohitaji kukabiliwa kwa mazingira ya dharura.

Akizungumza na Mwananchi kamanda wa kikosi hicho mkoani Kagera, Hamis Dawa  amesema wamefika mapema kwenye eneo la tukio na kushiriki kuzima moto na shughuli za uokoaji.

Ametaja baadhi ya changamoto zilizobainika kuwa ni uchache wa magari ya kusafirisha wagonjwa na  wataalamu wa afya katika hospitali walikopelekwa  majeruhi wa ajali hiyo.

Pia Soma

Chanzo: mwananchi.co.tz