Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mawe ya ajabu yashambulia nyumba

Mawe Ya Ajabu.jpeg Mawe ya ajabu yashambulia nyumba

Sun, 18 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katika hali isiyokuwa ya kawaida Familia tatu katika Mtaa wa Uwanja Mkoani Geita zimekuwa zikishambuliwa kwa mawe nyakati za usiku na mchana huku mawe hayo yakiwa hayajulikani yanakotokea, baadhi yao huumizwa kwa mawe na mengine kuvunja vioo vya nyumba.

Mmiliki wa nyumba mbili ambaye mawe yamekuwa yakirushwa katika nyumba zake, Vicent Kisandu amekiri kubomolewa vioo katika nyumba yake anayoishi pamoja na nyumba aliyopangisha na kusema mirusho hiyo ya mawe imedumu kwa kipindi cha wiki mbili sasa na haijulikani inatoka wapi na nani anayerusha.

"Tukio hili limeanza taratibu sana tangu lilivyoanza lilianza kwenye nyumba ya Wapanagaji wakawa wanaona tuu mawe yanarushwa kwenye bati wakawa wanafuatilia kwamba ni kitu gani, tuliendelea na utaratibu wa kufanya doria kama kuna Mtu anarusha mawe hatukuweza kumpataā€¯

Diwani wa Kata ya Nyankumbu John Mapesa amekiri kuwepo kwa vitendo hivyo huku vikihusishwa na imani za kishirikina na kuwataka wanaofanya hivyo kuacha mara moja kwani wanahatarisha amani ya Mtaa huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live