Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mawaziri watua Mbeya kutatua mgogoro wa ardhi

41949 Mawaziripic Mawaziri watua Mbeya kutatua mgogoro wa ardhi

Sat, 16 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mbarali. Jopo la mawaziri limewasili mkoani Mbeya kwa ajili ya kushughulikia mgogoro wa mipaka katika  vijiji 32 vinavyopakana na Hifadhi ya Taifa ya Ruaha wilayani  Mbarali mkoani Mbeya.

Mawaziri hao ni Waziri wa Ardhi,  Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi; Waziri wa Maliasili na Utalii,  Dk Hamisi Kigwangalla; Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa na Waziri wa Tamisemi, Seleman Jafo.

Wengine ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi;  Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Musa Sima na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina.

Mawaziri hao wanatarajiwa kutembelea eneo lenye mgogoro huo kabla ya kuzungumza na wananchi ili kuona namna wanavyoweza kufikia azma ya kurasimisha vijiji hivyo.

Inadaiwa vijiji hivyo vipo ndani ya hifadhi kwa mujibu wa Tangazo la Serikali namba 28 la mwaka 2008 (GN No.28 ya 2008), hivyo wamekuwa kwenye mgogoro kwa muda wa miaka 12.

Januari 15, 2019, Rais John Magufuli aliagiza vijiji vyote 366 vilivyobainishwa kuwepo ndani ya maeneo ya Hifadhi za Taifa nchini visiondolewe na badala yake wizara husika zianze kufanya mchakato wa kuvirasimisha huku akitoa muda wa mwezi mmoja kwa viongozi kubainisha maeneo ya vijiji hivyo na kuanzisha mchakato wa mabadiliko ya sheria ili yawasilishwe katika kikao kijacho cha Bunge.



Chanzo: mwananchi.co.tz