Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mawaziri sita kukutana na wafanyabiashara, wawekezaji Mtwara

77203 Pic+mawaziri

Wed, 25 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mtwara. Jumla ya mawaziri na manaibu waziri sita wanatarajiwa kukutana mkoani Mtwara nchini Tanzania leo Jumatano Septemba 25, 2019 kwa ajili ya kukutana na wafanyabiashara na wawekezaji  ili kufahamu changamoto zinazowakabili  ili kuzitafutia ufumbuzi.

Mawaziri hao ni Angellah Kairuki (Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu- Uwekezaj), Innocent Bashungwa (Viwanda na Biashara) na Doto Biteko wa Madini.

Manaibu waziri ni; Angelina Mabula (Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi), Mussa Sima (Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira) na Subira Mgalu wa Nishati.

Aidha washiriki wengine wa kikao hicho ni Mkurugenzi wa Utafiti, Sera na Mipango kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Bunini Mafuta na wajumbe kutoka Chama cha Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo (TCCIA), baadhi ya wabunge, Jumuiya ya wafanyabiashara na baadhi ya wajasiriamali na viongozi wa kiserikali kutoka wilaya zote za Mtwara.

Endelea kufuatilia Mwananchi kwa habari zaidi

Chanzo: mwananchi.co.tz