Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mawasiliano yakatika Mikumi - Kilombero

Mawasiliano Yakatika Mikumi   Kilombero Mawasiliano yakatika Mikumi - Kilombero

Tue, 12 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watumiaji wa barabara ya Mikumi - Kilombero Mkoani Morogoro wamelazimika kukaa zaidi ya saa kumi 12 Barabarani Baada ya Bimu ya daraja la Muzombe namba (12) kupinda na kusababisha magari kushindwa kupita.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Machi 12,2024, Msimamizi Kitengo Cha Matengenezo ya Barabara na Madaraja (TANROADS) Mkoa wa Morogoro, Mhandisi Patrick Rambika amesema changamoto ya daraja kuwa na shimo ni mara baada ya mvua kubwa iliyopelekea kufurika kwa maji katika daraja hilo kutokana na mvua kubwa zinazoendela kunyesha.

Anasema tijihada za haraka za kurudisha mawasiliano katika eneo hilo zinaendelea na magari yataruhusiwa kupita mara baada ya matengenezo yatakayofanyika kwa zaid ya saa 4 hadi 5.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live