Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mawasiliano Barabara ya Mikumi – Kilombero yakatika

Kimikikmn Mawasiliano Barabara ya Mikumi – Kilombero yakatika

Tue, 12 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watumiaji wa Barabara ya Mikumi – Kilombero Mkoani Morogoro wamelazimika kukaa zaidi ya saa kumi 12 Barabarani baada Bimu ya Daraja la Muzombe 12 kupinda na kusababisha magari kushindwa kupita.

Msimamizi kitengo cha matengenezo ya Barabara na Madaraja wa TANROADS, Mhandisi Patrick Rambika amesema changamoto hiyo ilitokea baada ya Mvua kubwa iliyopelekea kufurika kwa maji.

Amesema, tijihada za haraka za kurudisha mawasiliano katika eneo hilo zinaendelea na Magari yataruhusiiwa kupita mara baada ya matengenezo yatakayofanyika kwa zaidi ya saa 4 hadi 5.

Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro, Dkt. Mussa Ally Mussa amewaondolea hofu watumiaji wa barabara na kusema Serikali ipo kazini kuhakikisha huduma hiyo muhimu ya usafiri na usafirishaji inarejea kwa wakati.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live