Wed, 22 May 2024
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Mawasiliano ya barabara katika eneo la Kilwa Masoko hadi Nangurukulu wilayani Kilwa na Liwale mkoani Lindi yamerejea.
Wakala ya Barabara nchini (TANROADS) mkoa wa Lindi umerejesha mawasiliano hayo kwa kujenga njia ya dharura ili kuruhusu shughuli za maendeleo kuendelea kufanyiba baada ya barabara ya awali kusombwa na mafuriko yaliyosababishwa na kimbunga Hidaya.
TANROADS imetatua changamoto hiyo kwa kujenga darajaa muda katika Mto Zinga unaotenganisha kijiji cha Zinga na Miguruwe.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live