Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mavunde atoa somo kwa wanawake

45606 Pic+mavunde Mavunde atoa somo kwa wanawake

Sun, 10 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Vijana, Antony Mavunde amewataka wanawake kupendana na kuacha kuoneana wivu wanapoona wenzao wamefanikiwa.

Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani leo Ijumaa Machi 8 2019, Mavunde amewataka kujifunza kutoka kwa watu waliofanikiwa.

"Mnawekeana makundi, kusengenyana na umbea acheni na badala yake mjifunze kutoka kwao. Si kama nawakosoa ila nataka mjirekebishe muweze akiendelea," amesema.

Amesema ili kuwawezesha wanawake kupata mifuko yenye nafuu ya riba wameliagiza Baraza la Uwezeshaji nchini kutembea na kufanya makongamano kwa wananchi ili waweze kuifahamu mifuko ya uwezeshaji iliyopo.



Chanzo: mwananchi.co.tz