Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mavunde amkalia kooni mkandarasi Katavi

Mavunde Kl Mavunde amkalia kooni mkandarasi Katavi

Wed, 11 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naibu Waziri wa Kilimo, Anthony Mavunde, amempa siku 14 mkandarasi anayetakiwa kukarabati mradi wa umwagiliaji wa Kilida uliopo Kijiji cha Kilida, kilichopo Jimbo la Kavuu, Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe, mkoani Katavi, awe amefika eneo la kazi.

Mavunde ametoa maelekezo hayo alipotembelea mradi huo kujionea uharibifu uliotokana na mvua kubwa zilizonyesha na kuharibu baadhi ya mashamba ya wakulima katika kijiji hicho.

“Nimewaelekeza Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kuhakikisha mkandarasi anayetakiwa kujenga mradi huu awe amefika hapa ndani ya siku 14 kuanzia tarehe ya leo,” amesema na kuongeza:

“Awali mkandarasi alikuwa anasema anashindwa kufika kwa sababu ya mvua, ila nimefika mwenyewe mpaka hapa na nimejionea barabara zinapitika na hamna kisingizo, nampa siku 14 aje aanze kazi tuwasaidie wananchi wetu,” amesema.

Amesema serikali imejipanga vizuri kuhakikisha inaongeza wigo wa kilimo cha umwagiliaji mchini, ili kufikia malengo waliyojiwekea ya kukuza sekta ya kilimo kwa asilimia 10, ifikapo mwaka 2030.

Awali Mbunge wa Jimbo la Kavuu na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Geophrey Pinda, amesema kuwa mradi huo wa umwagiliaji utakapojengwa na kukamilika licha ya kutoa ajira utasaidia pia kuzalisha mbegu.

“Tunataka hapa pawe na mradi mkubwa wa umwagiliaji utakaosaidia uzalishaji mkubwa wa mbegu. Wananchi wa huku wanaumizwa sana na bei ya mbegu, ila zikizalishwa hapa maisha ya wananchi wengi hapa yatabadilika,” amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live