Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mavunde aagiza maeneo yapimwe

MAVUNDEEEEEE Naibu Waziri wa Kilimo, Anthony Mavunde

Thu, 20 Oct 2022 Chanzo: eatv.tv

Naibu Waziri wa Kilimo, Anthony Mavunde, amezitaka taasisi zote zilizo chini ya Wizara ya Kilimo kuhakikisha zinayapima maeneo yao ili kupata hati za umiliki wa ardhi na pia kuweka uzio katika maeneo yote ili kupunguza migogoro isiyo ya lazima na kupunguza uvamizi wa maeneo hayo.

Naibu Waziri Mavunde ameyasema hayo mkoani Mwanza wakati wa kikao cha utatuzi wa migogoro ya ardhi ya vijiji 975 inayoshughulikiwa kamati ya Mawaziri nane wa kisekta ambapo kamati hiyo ilikuwa katika Kata ya Shibula,Wilaya ya Ilemela-Mwanza.

"Ni wakati muafaka sasa taasisi zote zilizo chini ya Wizara ya Kilimo kuhakikisha mnayalinda na kuyatunza maeneo yenu kwa kuyapima na kuzungushia uzio, kuyaacha mashamba haya bila kuyatumia kwa eneo kubwa kunasabisha uvamizi wa maeneo haya ambayo mengi yametengwa kwa ajili ya uzalishaji mbegu na utafiti wa kilimo," amesema Naibu Waziri Mavunde

Aidha Mavunde ameongeza kuwa, "Hivyo naagiza taasisi zote kuhakikisha mnatenga bajeti ya kulinda haya maeneo na kusimamia malengo ya  matumizi yake, Mh.Rais Samia Suluhu Hassan ametuongezea bajeti kwenye wizara yetu hivyo hakikisheni katika mipango yenu inahusisha ulinzi wa maeneo haya,"

Chanzo: eatv.tv