Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mauti yamfika akishindana kunywa Pombe

Pombe Battle Mauti yamfika akishindana kunywa Pombe

Wed, 21 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtu mmoja aitwaye Ben amefariki dunia na wengine wanne wamelazwa katika eneo la Sanyajuu Wilaya ya Siha Mkoani Kilimanjaro baada ya kunywa pombe ya mashindano ambayo Mshindi wa kunywa chupa 8 za pombe kali alikuwa akipewa shilingi elfu 50, mkate na sukari.

Feliz Mrema Shuhuda wa tukio hilo amesema kuwa Mtu mmoja anayefahamika kwa jina la Dkt Shika alikuwa akisherehekea siku yake ya kuzaliwa na kutoa ofa kwamba atakayemaliza chupa nne atapewa sukari kilo moja huku atakayemaliza chupa nane akiahidiwa kupewa sukari, mkate na shilingi elfu 50.

“Ben alivyokuja alikunywa na hakufikisha hata vinne palepale aliishiwa nguvu na kudondoka”

Mkuu wa Wilaya ya Siha Christopher Timbuka amesema tukio ni la kweli na kwamba Mtu mmoja alifariki na wengine kukimbizwa Hospitali kwa ajili ya matibabu na hali zao zinaendelea vizuri.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live