Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mauaji yatikisa wilayani Serengeti

SERENGETI Mkuu wa wilaya ya Serengeti, Dk Vicent Mashinji

Tue, 21 Sep 2021 Chanzo: Mwananchi

Watu sita wamefariki baada ya kujeruhiwa na visu na mapanga katika matukio tofauti yaliyotokea katika Wilaya ya Serengeti mkoani Mara.

Matukio hayo yametokea katika kipindi cha miezi mitatu katika maeneo ya sterehe.

Azikungumza mjini Mgumu leo Septemba 21, 2021 katika uzinduzi wa ofisi ya Taifa ya mashtaka ya Wilaya ya Serengeti, mkuu wa wilaya hiyo, Dk Vicent Mashinji amesema zipo hatua mbalimbali zilizochukuliwa na uongozi wa wilaya kuhakikisha matukio ya mauaji yanapungua katika wilaya hiyo.

Amesema hatua hizo ni pamoja na kupiga marufuku ubebaji wa visu na mapanga katika sehemu za starehe kwa maelezo kuwa wenye silaha hizo imeelezwa kuwa muda wowote wanaweza kutekeleza mambo maovu.

"Tumegundua ubebaji holela wa mapanga na visu katika sehemu za starehe ni kichocheo cha matukio haya kwani kuna watu wanashindwa kuhimili kiwango cha kilevi, wanafikia hatua ya kutumia silaha hizo kudhuru na hata kuua pale inapotokea wametofautiana kauli, " amesema.

Amesema kutokana na ubebaji huo holela wa silaha, matukio ya mauaji katika Wilaya ya Serengeti yamekuwa mengi hali inayotakiwa kukomeshwa.

Amebainisha uwepo wa ofisi hiyo utasaidia mapambano ya mimba za utotoni wengi wakiwa wanafunzi.

Mkurugenzi mkuu wa Mashtaka nchini(DPP), Sylvester Mwakitalu amesema hadi kufikia Septemba 10, 2021 wilaya ya Serengeti ilikuwa na kesi 29 za mauaji ambapo kesi 25 ni za mauaji ya kukusudia huku kesi nne zikiwa ni za mauaji ya bila kukusudia.

Chanzo: Mwananchi