Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Matajiri watajwa kufukua makaburi, kuiba viongo vya maiti

Makaburi Mes Matajiri watajwa kufukua makaburi, kuiba viongo vya maiti

Mon, 17 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Mkoani Singida limesema uchunguzi wao umebaini baadhi ya matajiri wanahusika katika kuwezesha na kufadhili Mauaji ya Watu, Wizi wa Mali kwa kuwalipa wanaofukua makaburi yaliyopo Wilaya ya Manyoni

Kamanda wa Polisi Mkoa, Stella Mutabihirwa, amesema tayari watuhumiwa 13 wamekamatwa na uchunguzi umeonesha wanatumwa na baadhi ya matajiri wanaotaka kulinda utajiri wao au kupata utajiri kwa imani za Kishirikina

Jeshi la Polisi limefanya mahojiano na watuhumiwa ambao wamekiri kutumwa na baadhi ya Matajiri kwa maagizo ya Waganga wa Kienyeji ambao huwaagiza kupeleka viungo vya Watu na viambata vya Maiti, ambavyo hupatikana kwa kufukua makaburi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live