Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mashamba mengine ya bangi yafyekwa Tarime

Mashamba Ya Bangi (600 X 359) Mashamba mengine ya bangi yafyekwa Tarime

Tue, 17 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa mkoa wa Mara, Said Mtanda ameongoza Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa huo kufyeka zaidi ya heka tatu za mashamba ya bangi.

Zoezi hilo limefanyika katika kijiji cha Nkerege wilayani Tarime, zikiwa zimepita siku chache tangu kufyekwa na kuchomwa moto ekari 807 za bangi katika bonde la mto Mara.

Mtanda amesema Serikali inaangalia namna ya kubadili matumizi ya bonde hilo kama njia ya kutokomeza kilimo cha bangi.

Kijiji cha Nkerege ni miongoni mwa vijiji vilivyo ndani ya Bonde la mto Mara, ambavyo vimekuwa vikijihusisha na kilimo cha bangi kwa muda mrefu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live