Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mashahidi kesi ya Mfalme Zumaridi wakana maelezo ya Polisi

Zumaridipiic Mashahidi kesi ya Mfalme Zumaridi wakana maelezo ya Polisi

Sat, 26 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mashahidi watatu wa utetezi katika kesi namba 10/2022 ya kuwazuia maafisa wa serikali kutekeleza majukumu yao na kuwashambulia askari polisi wawili inayomkabili Diana Bundala maarufu kama Mfalme Zumaridi na wafuasi wake 8 wametoa ushahidi wao katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Mwanza.

Mashahidi hao ni Neema Julian ambaye ni mshitakiwa namba 5, Geoge Maloji ambaye ni  mshitakiwa namba 8,  pamoja na Isaka Mashaka mshitakiwa namba 4 katika kesi hiyo.

Akitoa ushahidi wake Neema Julian ameieleza mahakama kuwa yeye hujishughulisha na usafi  nyumbani kwa Mfalme Zumaridi na kwamba siku ya Februari 23/2022 hakujua kilichotokea kwani alikuwa akimwagilia maua nje ndipo akaona gari la polisi likiingia nyumbani kwa Zumaridi na kuwakamata 

Aidha ameieleza mahakama kuwa  maelezo  yaliyowahi kutolewa makamani kama ushahidi si yake kwani aliyakuta mahakamani hivyo  anachokumbuka akiwa polisi aliulizwa majina yake, umri, kazi yake na mahala anapoishi.

Shahidi mwingine George Maloji ameieleza mahakama hiyo kuwa alikamatwa Februari 26 mwaka huu akiwa nyumbani kwa Zumaridi akiuza nguo kwani yeye ni  machinga hivyo alifika hapo siku hiyo kwa lengo la kutafuta wateja wa biashara yake.

Ameongeza kuwa anakumbuka siku ambayo Inspekta Zongo alitoa ushahidi wake alidai mahakamani hapo kuwa anamtabua kwa kuwa alimwandika maelezo lakini alishangazwa na kitendo cha kuionyesha mahakama maelezo yasiyo na jina lake baali yana jina lingine.

Naye Isaka Mashaka fundi ujenzi akitoa ushaidi wake ameieleza mahakama kuwa kabla ya kukamatwa Februari 26, 2022 alisikia kishindo cha geti kuvunjwa pamoja na milio ya risasi ndipo akakamatwa na Askari polisi na  kuacha kazi yake ya ujenzi iliyompeleka nyumbani kwa mhubiri huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live