Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Masanja atoa maagizo kwa wananchi Tarime

Masanja Utalii Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mary Masanja

Mon, 8 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imewataka wananchi wilayani Tarime mkoani Mara kuheshimu maeneo ya hifadhi kwa kuacha kufanya shughuli za kibinadamu katika maeneo hayo.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mary Masanja, amesema hayo katika Kijiji cha Gibaso Kata ya Kwihancha wakati wa ziara ya Mawaziri Watatu kutoka Ofisi ya Rais- TAMISEMI, Wizara ya Ardhi, pamoja na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa ajili ya kusikiliza kero za wananchi wanaoishi pembezoni mwa Hifadhi ya Serengeti.

Amesema kuwa mwananchi yeyote haruhusiwi kukanyaga hifadhini, kutokana na kuwepo kwa wanyama wakali na changamoto za majangili

"Nimesikia hapa kuna malalamiko mengi pindi mnapoingia ndani ya Hifadhi, naomba kuwaeleza kuwa eneo lile linatunzwa kwa sheria za nchi na hairuhusiwi kufanya shughuli zozote za kibinadamu," amesema Naibu waziri Masanja

Aidha, amefafanua kuwa kazi ya Askari wa Uhifadhi walio katika maeneo ya Hifadhi ni kulinda Hifadhi pamoja na rasilimali zilizomo hifadhini na si vinginevyo.

Amewaasa wananchi hao kuacha tabia ya kuwalaumu Askari Uhifadhi na badala yake waheshimu sheria za nchi kwa kuacha kuingia katika maeneo hayo

Mhe. Masanja amewataka wananchi kukaa katika maeneo ya vijiji yanayoruhusiwa kwa shughuli za kibinadamu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live