Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Marufuku mifuko ya plastiki yapamba moto

Matumizi Ya Mifuko Ya Plastiki 660x400.jpeg Marufuku mifuko ya plastiki yapamba moto

Sat, 22 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera ametanga kuanza operesheni maalum ya kukamata watu wanaojihusisha na biashara ya uzalishaji na usambazaji wa mifuko ya plastiki iliyopigwa marufuku na Serikali.

Homera ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Oktoba 21, 2022 wakati wa akizindua kampeni ya kutokomeza mifuko ya plastiki liliyofanyika katika Stendi ya Kabwe jijini Mbeya.

“Kumekuwepo na uzalishaji mkubwa na utupaji holela wa mifuko ya plastiki ambayo imepigwa marufuku na Serikali sasa itafanyika operesheni maalum ya kuwasaka wazalishaji na wasambambaji sambamba na wafanyabiashara wa rejareje,” amesema.

Amesema kuwa uwepo wa mifuko hiyo inasababisha uchafuzi wa mazingira na kusababisha maeneo mengi kuwa katika hali ya uchafu uliokithiri.

“Shirika la Viwango nchini (TBS) toeni elimu kwa wananchi hususan kwa wafanyabishara kuhusiana madhara ya matumizi holela ya mifuko ya plastiki kuhifadhia chakula,” amesema.

Amesema kukosekana kwa elimu ni changamoto kubwa ambayo inasababisha wananchi kukiuka maagizo ya Serikali na kupelekea kushamili wa uuzwaji holela wa mifuko ya plastiki Jijini hapa.

Homera amesema kuwa wakati Serikali ikiendelea na oparesheni ya kuwasaka wazalishaji TBS waendelee kutoa elimu ya athari ya matumizi ya mifuko ya plastiki ambayo imepigwa marufuku na serikali kutokana na kuwepo kwa madhara kwa watumiaji.

“Nasisitiza kwa wazalishaji ambao watabainika hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao kwani Serikali haiwezi kuvumilia watu wanaokwenda kinyume na maagizo ya makatazo yanayotolewa mara kwa mara,” amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live