Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Marais wastaafu waombwa kujadili kikokotoo kipya cha mafao

31458 Kikoootopic TanzaniaWeb

Thu, 13 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mbeya. Chama cha Kutetea Haki na Maslahi ya Walimu Tanzania (Chakamwata) kimeiomba Serikali kuwakutanisha na watumishi wa umma wakiwamo marais wastaafu ili kujadili sheria na kanuni mpya ya kikokotoo cha mafao ya pensheni kwa wastaafu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Mbeya leo Alhamisi Desemba 13, 2018, Katibu Chakamwata Tanzania, Meshack Kapange amesema sheria hiyo imepitishwa bila kuwashirikisha watumishi wa umma badala yake walitumia vyama vya wafanyakazi ambavyo havina nia njema na watumishi wa umma.

Kapange amesema wamekuwa wakipinga kikokotoo hicho mara kwa mara wanapokutana na  viongozi mbalimbali wa Wizara ya Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) kwa kuwaeleza ni kwa namna gani fomula hiyo inawakandamiza walimu na watumishi wa umma kwa ujumla.

"Tunaomba mjadala wa kikokotoo kipya kutokana na kwamba kinamfanya mtumishi Serikali ngazi ya kawaida kuwa maskini zaidi, mbaya zaidi kikokotoo hicho hakijawagusa wastaafu wa kisiasa kama    Rais, wabunge na madiwani ambao wanatumikia kwa muda mfupi wanachukua pensheni zao kwa asilimia 80, sasa kwa nini watumishi wa umma tuchukue asilimia 25",alisema Kapange.

Kapange alifafanua kuwa mjadala wa kikokotoo baina ya Serikali na watumishi wa umma nchi itageuka nchi ya wanasiasa badala ya wananchi wanyonge.

Makamu Mwenyekiti wa Chakumwata taifa, Juma Issa amesema Serikali isitishe sheria Mpya ya kikokotoo hicho kwa masilahi mapana ya nchi kwani bila kufanya hivyo ni kuendelea kuwakandamiza wananchi.

“ Tunapoingia kwenye mjadala huu mpana naomba Serikali iendelee kutumia kikokotoo kile cha zamani kwa wastaafu wa sasa na wa badaye, itasaidia kufuta kilio cha mfanyakazi ni kilio cha nchi nzima kwani wasiyo watumishi wanaishi kwa kutegemea watumishi," amsema Issa.

Mwenyekiti wa chama hicho Wilaya ya Mbarali, Moses Mwalyego, amesema kanuni hiyo mpya watumishi wanapaswa kuungana kupinga sheria hii kandamizi kwa wafanyakazi bila kujali itikadi za vyama vyao kwani kila mmoja ni mstaafu mtarajiwa.

Soma Zaidi: Wadau wahoji matumizi faida ya uwekezaji wa hifadhi ya jamii



Chanzo: mwananchi.co.tz