Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mapya yaibuka vifo vya watoto watano Monduli

0065fc1dfc1e2de9165b51a48bf3d501 Mapya yaibuka vifo vya watoto watano Monduli

Wed, 20 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Frank Mwaisumbe ametoa rai kwa jamii za kifugaji kuacha kutumia mitishamba isiyodhibitishwa na Wizara ya Afya.

Mwaisumbe ametoa rai hiyo leo, wakati wa kuaga miiili ya watoto watano wa familia moja waliofariki kutokana na kunywa kitu kinachodhaniwa kuwa na sumu.

Mwaisumbe amesema watoto hao wa familia moja wakiwemo wanne waliofariki kwa nyakati tofauti katika hospitali ya Mount Meru na mwingine watano aliyetangulia kufariki aitwaye Bosii Nyangusi, aliyezikwa Jumapili kijijini kwao Mswakini kata ya Mswakini Wilayani Monduli, mkoani Arusha.

Amesema sampuli za awali zilizochukuliwa zimebainisha watoto hao walikunywa au kula chakula chenye sumu na sampuli hizo zimepelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali Dodoma na baada ya wiki mbili majibu yatatolewa.

Amesema wazazi wa watoto hao wanashikiliwa na jeshi la polisi na majibu ya sampuli yakitoka na ikidhibitika ni simu walipewa hatua za kisheria zitachukuliwa.

Watoto hao waliofariki ni Bosii Nyangusi (14) mwanafunzi wa darasa la sita shule ya msingi Mswakini na Veronica Nyangusi (10) mwanafunzi wa shule hiyo, pacha wawili Lenendoye na Lemali miaka (8) na Sofia.

Kwa mujibu wa Mwaisumbe, alisema kuna taarifa fiche za utata wa vifo vya watoto wao kwani, awali Bosii alipoanza kuumwa alikimbizwa mkoani Babati, hajulikani alipelekwa kwa ajili gani kisha wakamtoa na kumpeleka hospitali ya Karatu kwa matibabu zaidi na baadaye alifariki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live