Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mapunda amuua kwa panga ex wake, naye ajinyonga

PANGA Ed Mapunda amuua kwa panga ex wake, naye ajinyonga

Tue, 19 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Doto Hamisi Magambazi, mwanamke mwenye umri wa miaka 30, mkazi wa Mjimwema Kiluvya mkoani Pwani amefariki dunia, wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Tumbi, baada ya kushambuliwa kwa kukatwa na panga sehemu mbalimbali za mwili wake.

Kulingana na taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani, imeeleza kuwa baada ya uchunguzi wa awali uliofanywa na Jeshi hilo, ilibainika kuwa aliyehusika na shambulio hilo ni mume wake, aitwaye Mbaraka Haruna Mapunda (42), mkazi wa Chanika mkoani Dar es Salaam, aliyetalakiana nae mwaka mmoja uliopita, huku chanzo kikitajwa kuwa ni wivu wa mapenzi na kugombea mali walizochuma pamoja.

Wakati Jeshi hilo likiendelea na msako wa kumakamata mtuhumiwa, ilibainika kuwa Mtuhumiwa huyo alikuwa amejinyonga umbali wa mita 300 kutoka nyumbani kwa Bi.Doto Magambazi, Mtaa wa Mjimwema Kiluvya, kwenye kichaka kwa kutumia mkanda wa nguo kwa kujininginiza kwenye mti.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live