Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maporomoko ya Kalambo yalivyoibua fursa mpya utalii

Maporomoko Utalii.png Maporomoko ya Kalambo yalivyoibua fursa mpya utalii

Tue, 5 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Miongoni mwa vivutio vya utalii visivyo na umaarufu nchini ni maporomoko ya maji ya moto Kalambo yaliyopo mkoani Rukwa.

Ni maporomoko ya pili kwa urefu barani Afrika yapo kwenye mpaka wa Zambia na Tanzania yakifuatia ya Tugela yaliyopo katika milima ya Drakensberg nchini Afrika Kusini.

Pamoja na kwamba maporomo ya Kalambo yapo katika nchi mbili, watalii wengi wanapendelea upande wa Tanzania kwa sababu maji yanaonekana, ambayo pia huongeza thamani ya eneo hilo.

Kutokana na umuhimu wake kiuchumi, miundombinu wezeshi imejengwa kisasa na inachangia kuongezeka kwa idadi ya watalii wanaotembelea eneo hilo.

Kutokana na sababu hiyo, wadau wa utalii wanatoa wito kwa wawekezaji kuwekeza kwenye utalii wa kambi ili kuwawezesha watalii kulala badala ya kuja na kuondoka siku hiyo hiyo.

Akizungumzia na waandishi wa habari wakati wa ziara katika eneo hilo hivi karibuni, ofisa mwongoza watalii kutoka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Sadoki Nsekela anasema eneo hilo limejengwa kwa ngazi zaidi ya 1,200 zinazowawezesha watalii kushuka na kupanda kwa urahisi, pia kuna vituo vitatu kabla ya kufika.

Ziara hiyo iliandaliwa na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) chini ya mradi wa Resilient Natural Resource Management for Tourism and Growth Project (Regrow) unaolenga kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo mikoa ya kusini.

"Miundombinu hii wezeshi imechangia kuongezeka kwa idadi ya watalii hadi 2,500 kwa mwaka kutoka chini ya watalii 500 katika miaka minne iliyopita kutoa wito kwa wawekezaji kuwekeza katika kambi.

"Miundombinu hii wezeshi imechangia kuongezeka kwa idadi ya watalii hadi 2500 kwa mwaka kutoka chini ya watalii 500 katika miaka minne iliyopita kutoa wito kwa wawekezaji kuwekeza katika kambi," anesema.

Mbali na hayo, anasema watalii wanapofika katika eneo hilo, hufurahia miundombinu kwa sababu wanaweza kuona asili katika eneo hilo.

Kadhalika amesema kufika katika eneo hilo kuna vituo vitatu ambavyo maji yanaonekana kwa asilimia 45, 75 na 100 hivyo mtalii huamua wapi aishie kutokana na mpangilio huo.

Mkazi wa kijiji cha Kalambo, Jeremiah Lukas anasema katika kipindi hiki cha watalii idadi kubwa ya magari na makundi ya watu hutembelea eneo hilo, japo wengi bado hawajaweza kutumia fursa hiyo.

"Mimi ni mkulima katika eneo hili, huwa naingia na kuondoka, wenyeji bado hawajaweza kutumia fursa kama vile kufungua migahawa kwa wageni kula, lakini natumai siku hadi siku mambo yatabadilika," amesema.

Kwa upande wake, Ofisa Uhusiano wa TTB, Augustina Makoye alisema kuna vivutio vingi vya utalii katika mikoa ya kusini, bado havijatumika kama vile maporomoko ya maji, maziwa na mbuga za wanyama.

Amesema mradi wa kukuza upya miongoni mwa mambo mengine ni kutangaza vivutio hivyo duniani kote

Chanzo: www.tanzaniaweb.live