Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mapato yaongezeka Bandari ya Kigoma

90a01195f73743b8c9e4e0443fe4557f Mapato yaongezeka Bandari ya Kigoma

Sat, 6 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania, Mhandisi Deusidedit Kakoko amesema kuwa Bandari ya Kigoma imeanza kutoa matokeo chanya kwa kuongezeka idadi ya shehena za mizigo pamoja na mapato baada ya kufanyiwa maboresho makubwa.

Kakoko amebainisha hayo mkoani humo alipotembelea bandari hiyo na kuongeza kuwa mapato yake yameongezeka kuipita Bandari ya Mwanza iliyokuwa ikiongoza mara baada ya kuboreshwa.

“Bandari ya Kigoma inahusisha bandari zote zilizopo katika Ziwa Tanganyika na ilianza kufanyiwa marekebisho toka mwaka 2016 katika maeneo yake mbalimbali na kwa sasa ipo katika hatua za mwisho kabla ya kukamilika kwake lakini tayari imeanza kutoa matokeo chanya” amesema Kakoko.

Chanzo: www.habarileo.co.tz