Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mapato kituo cha mabasi yaponza Wafanyakazi wa Jiji la Arusha

Mapato kituo cha mabasi yaponza Wafanyakazi wa Jiji la Arusha

Wed, 27 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arusha. Mkurugenzi  wa  Halmashauri ya Jiji la Arusha, Dk Maulid Madeni amemsimamisha kazi Mkuu wa Idara ya Mipango Miji na Ardhi, Dickley Nyato na Ofisa Mipango Takwimu na Ufuatiliaji (Mchumi), Anna Mwambene ili kupisha uchunguzi wa eneo la ujenzi kituo cha mabasi lililopo eneo la Bondeni City ekari 30.

Akizungumza na Waandishi  wa habari leo Jumatatu Novemba 25, 2019, Dk Madeni amesema baada ya halmashauri kubaini ubadhirifu wa Sh1.9 bilioni za ununuzi wa eneo la ekari 29.5 lililopo Mtaa wa Oloresho Kata ya Olasiti na kukataa kulipa fidia, wananchi waliamua kutafuta ekari 30 za bure zilizopo eneo la Bondeni City katika Kata hiyo.

“Eneo hili lilifanyiwa tathimini huko nyuma na muhtasari uliandikwa Februari 24 mwaka 2017 ukitutaka tulipe fidia Sh.bilioni 1.1 lakini mwaka huo huo Machi 6 ukaandikwa muhtasari mwingine ukitaka tulipe Sh.bilioni 1.9 sasa mimi nikakataa,” amesema.

Amesema kutokana na mvutano huo, alifanya uchunguzi na kuwataka wakuu hao wa idara kumuandikia barua za kujieleza juu ya mamlaka ya kubadilisha maamuzi ya Baraza walikopata na kuongeza kiasi hicho cha fedha.

Kwamujibu wa Dk Madeni, waliandika barua zao na kumpelekea Novemba 19, mwaka huu, lakini baada ya kuzisoma hakuridhika na sababu zao na kuwasimamisha kazi kupisha uchunguzi dhidi yao.

Chanzo: mwananchi.co.tz