Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maonesho ya Nanenane yaondolewe Dodoma - Mbunge CCM

KISANGI TZW

Thu, 7 Jun 2018 Chanzo: --

Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Mariamu Kisangi , ameitaka Serikali kuondoa Maonyesho ya Wakulima Nanenane Dodoma kwa maelezo kuwa mkoa huo sasa umekuwa Jiji. Mariamu ametoa kauli hiyo leo Juni 7, 2018 bungeni mjini Dodoma katika kipindi cha maswali ya papo kwa hapo kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Katika swali lake, mbunge huyo amesema haitakuwa na tija kwa sasa kuwa na maonyesho ya wakulima katika eneo ambalo limekuwa jiji wakati dhima ya maonyesho hayo ni wakulima kujifunza. Katika majibu yake Majaliwa amesema hakuna sheria ya kuondoa maonyesho hayo katika majiji kwa maelezo kuwa yapo mengine ambayo maonyesho hayo yanafanyika.

“Wakati fulani niliwahi kuwa mgeni rasmi katika maonesho kama hayo jijini Mbeya, hivyo kwamba maonesho yaondolewa sio kigezo muhimu kwa sasa labla pale Waziri wa Kilimo atakapoona inafaa,” amesema Majaliwa.

kwa upande wake mbunge wa Longido, Dk Stephen Kiruswa ameitaka Serikali kutoa tamko ni lini itazifuta NGOs zinazokiuka masharti na kuhamasisha migogoro.

Chanzo: --