Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maofisa mazingira wapewa neno uchafuzi wa mazingira

4351729174791a1d39ce738a394526dd Maofisa mazingira wapewa neno uchafuzi wa mazingira

Mon, 24 Aug 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MKURUGENZI Mkuu wa Baraza la Usimamizi wa Mazingira Taifa (NEMC), Dk Samweli Gwamaka, amewataka mao? sa mazingira nchini kuwajibika ili kupunguza uchafuzi wa mazingira nchini.

Dk Gwamaka na Mwenyekiti wa Bodi ya NEMC, Profesa Esnati Chaggu, wamemaliza ziara ya kutembelea mikoa ya Kusini mwaTanzania, ambapo ametaka maofisa hao wasimamie ulinzi wa mazingira kuanzia ngazi ya kijiji hadi mkoa.

“Kumekuwa na uzembe unaofanywa na maofisa wetu wa mazingira kwenye maeneo mbalimbali nchini kwa kushindwa kutimiza majukumu yao.

Wakati umefika kubadilika na kufanya kazi ipasavyo. Watumishi wasipotimiza wajibu wao na ukatokea uchafuzi wa mazingira ni jamii ndiyo inaathirika,” alisema.

Dk Gwamaka aliwataka maofisa hao kupeleka ripoti zao ofisi za NEMC na Ofisi ya Makamu wa Rais, Kitengo cha Mazingira kuhusu maeneo wanayoyasimamia kwani ni kati ya vigezo vya utendaji wao kazi.

Alisema changamoto za kimazingira zisipotatuliwa, afya za watu zinaweza kuathirika na uchumi wa taifa kudhoofika. Dk Gwamaka alionya kwamba, NEMC itawachulia hatua maofisa ambao hawatawajibika katika maeneo yao.

Chanzo: habarileo.co.tz