Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maofisa kilimo, wakulima wa korosho Moshi wapewa neno

7c58ce80bfa42ea865e75a870b218c29 Maofisa kilimo, wakulima wa korosho Moshi wapewa neno

Mon, 23 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MAOFISA kilimo na wakulima wa zao la korosho wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro wametakiwa kusambaza vizuri na kwa kasi kubwa elimu inayotolewa na wataalamu wa zao hilo kuhusu kupanda mbegu bora za korosho ili kuleta mafanikio chanya ya kilimo hicho wilayani humo.

Kauli hiyo ilitolewa hivi karibuni na Mrakibu Mwandamizi wa Gereza kuu Karanga, Frank Mwakijungu wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro wakati wa mafunzo ya siku mbili kwa wakulima wa zao la korosho.

Mafunzo hayo ni kuhusu kilimo bora cha zao la korosho na ubora wake yanayoendeshwa na Bodi ya korosho Tanzania(CBT) kwa kushirikiana na TARI Naliendele, lengo likiwa kuwapatia wakulima hao teknolojia mpya za kilimo bora cha zao la korosho kwa kupanda mbegu bora na kudhibiti wadudu waharibifu na magonjwa katika zao hilo.

Alisema wenye jukumu la kuifanya elimu hiyo kuweza kusambaza kwa kasi au kuwafikia kikamilifu wakulima na wadau wengine na korosho ni maofisa kilimo pamoja na wakulima ambao wameshiriki mafunzo wilayani humo.

Kwa upande wake mtaalamu kutoka TARI Naliendele, Dadili Majune alisema wakulima wilayani humo baada ya kupokea mbegu nyingi kutoka Tari Naliendele wamehamasika kupanda mikorosho lakini walikuwa na tatizo la namna ya kudhibiti wadudu waharibifu ambao ni mbu wa mikorosho na mbu wa minazi pamoja na magonjwa na baada ya kuletewa elimu hiyo wamefurahishwa kwani itawasaidia na kuongeza tija kwenye zao la korosho.

Chanzo: habarileo.co.tz