Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Manyara wapelekana mbio madarasa kidato cha kwanza

2a2edb79dae290516d3badd672b8f67f Manyara wapelekana mbio madarasa kidato cha kwanza

Mon, 21 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

KATIBU Tawala wa Mkoa wa Manyara, Musa Missaile ameziagiza halmashauri zote za mkoa huo kuhakikisha zinajenga madarasa pamoja na kutengeneza madawati ili wanafunzi wote 557 waliokosa nafasi za kujiunga kidato cha kwanza 2021 katika shule za sekondari zilizopo mkoani Manyara wawe wamesharipoti shule ifikapo mwezi Februari 2021.

Missaile alisema hayo jana alipokuwa katika kikao cha uchaguzi wa wanafunzi wanaotakiwa kujiunga kidato cha kwanza mwaka 2021 kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara.

Alisema kati ya watahiniwa 30,800 waliofanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi ni watahiniwa 22,476 walifaulu sawa na asilimia 72.97 ya watahiniwa waliofanya mtihani na kufaulu na wanafunzi 21,919 sawa na asilimia 97.52 ya waliofaulu wakiwemo wavulana 10,090 na wasichana 11,829 watapata nafasi ya kuingia kidato cha kwanza huku wanafunzi 4,510 wakishindwa kujiunga kutokana na kutokufaulu.

Hata hivyo katibu tawala huyo aliwataka walimu kushirikiana na wazazi kwa karibu ili waweze kutatua matatizo yanayowakumba wanafunzi kiasi cha kushindwa kufanya vizuri kwenye masomo yao

Kaimu Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya Elimu, Lago Sillo alisema kuwa kati ya watahiniwa 31981(wavulana 15,143 na wasichana 16,838) walioanza darasa la kwanza mwaka 2014, watahiniwa 30,800 (wavulana 14426 na wasichana 16,374) walifanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi na watahiniwa 1181 (wavulana 717 na wasichana 464) hawakufanya mtihani kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo utoro, vifo, ugonjwa n.k

Alisema halmashauri ya mji wa Babati ndio iliyongoza kwa kufaulisha ambapo imefaulisha kwa asilimia 84.33 ikifuatiwa na halmashauri ya Mbulu mji ambapo ina asilimia 81.47, Babati wilaya asilimia 74.51, Simanjiro asilimia 71.83, kiteto 71.74, Mbulu wilaya 68.92 na ya mwisho ni halmashauri ya Hanang ambayo imefaulisha kwa asilimia 67.43.

Mkurugenzi wa halmashauri ya Mbulu Mji, Anna Mbogo alisema kuwa kuna haja ya kujitathmini kama mkoa kwani nafasi walioshika kitaifa nafasi ya 23 siyo nzuri hivyo ni lazima uwepo mkakati wa juu kupitia ofisi ya elimu mkoa kukaa na maofisa elimu kama kamati waweze kuangaalia ni mikakati gani inaweza kuvusha na kupandisha mkoa kwani mkoa umekuwa nyuma kwa kipindi kirefu hususani kwenye matokeo ya darasa la saba.

Chanzo: habarileo.co.tz