Naiman Metili (43) Mkazi wa Ilbour wilayani Arumeru Mkoani Arusha ambaye ni manusura wa ajali ya gari iliyosombwa na Mafuriko katika maeneo ya Kin'gori asimulia mkasa mzima wa tukio hilo.
Ajali hiyo iliyotokea Aprili 25, 2023 na kusababisha vifo vya watu wanne ndugu, Mke na watoto wa Naiman Metili wakati wakiwa kwenye gari Moja aina ya Noah yenye Namba za usajili T499-DMI katika safari ya kutoka Mkoani Arusha kuelekea Mkoani Kilimanjaro.
"Tulikwenda vizuri na safari yetu, tulipofika pale kwenye maji tukapaki pembeni karibu saa moja na nusu tukiwa na wenzetu tukisubiri maji yapungue, tukawa tukinywa kawaha kwenye gari langu.
"Baadaye God akaniambia anawahi oparesheni ya mama yake, akaondoka alikuwa na Noah akapita, baadaye ikafuata Alphard na gari nyingine ndogo,mimi nilikuwa kama wa 10 hivi.
"Nilivyofika katikati ya maji, nilisikia kishindo kikubwa sana, sikujua ni ni nini lakini ilikuwa taili ya mbele. Nikajaribu kuirudisha nyuma lakini ilinishinda ikaingia kwenye mtaro, mtoto akasema Mungu msaidie baba, pale ndipo ikawa mwisho," amesema Naiman Metili.