Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Manispaa Ya Kigamboni Yakabidhiwa Mradi wa Viwanja

MRADI 3?fit=640%2C453&ssl=1 Manispaa Ya Kigamboni Yakabidhiwa Mradi wa Viwanja

Sun, 4 Jul 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

Kamishna wa Ardhi Msaidizi Kanda ya Dar es Salaam, Idrisa Kayera akifafanua jambo mbele ya Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kigamboni, Ernest Mafimbo (Kulia) wakati wa makabidhiano ya mradi wa viwanja 20,000 lililopo Kigamboni  Dar es Salaam.

Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kupitia ofisi ya Kamishna wa Ardhi mkoa wa Dar es Salaam imekabidhi mradi wa viwanja 20,000 kwa halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni iliyopo Dar es Salaam ili iweze kusimamia na  kuendeleza eneo la mradi.

Hatua hiyo inafuatia maagizo ya Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi kutaka manispaa ya Kigamboni kukabidhiwa mradi huo ili kutunza eneo la mradi kwa mujibu wa mipangomiji ya wilaya ya kigamboni.



…Kayera akionesha ramani ya eneo la mradi wa viwanja 20,000 lililopo Kigamboni Dar es Salaam wakati alipokabidhi mradi huo.

Akizungumza wakati wa kukabidhi mradi huo wa viwanja 20,000 Dar es Salaam kwa Mstahiki Meya ya Manispaa hiyo Ernest Mafimbo, Kamishna wa Ardhi Msaidizi Kanda ya Dar es Salaam, Idrisa Kayera alisema, lengo la kukabidhi mradi ni kutaka manispaa ya kigamboni itunze eneo la mradi kwa mujibu wa mipangomiji sambamba na kuzuia uvamizi wa eneo hilo.

Awali kwa Kwa mujibu wa Kayera alisema, eneo la viwanja 20,000 katika manispaa hiyo kulikuwa na changamoto mbalimbali kama vile uvamizi wa maeneo ya wazi na kubainisha kuwa, kutokana na mamlaka ya upangaji kuwa chini ya halmashauri wizara iliona ipo haja ya kukabidhi mradi huo kwa halamshauri.

“Wizara imeona ikabidhi mradi huu kwa kuwa halmashauri ina nafasi nzuri ya kusimamia mipangomiji pamoja na kuendeleza miundo mbinu ambapo awali jukumu hilo lilikuwa likifaywa na wizara na tuzingatie mamlaka ya upangaji iko chini ya halmashauri,” alisema Kayera.



Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kigamboni, Ernest Mafimbo (wa pili kushoto) na Kamishna wa Ardhi msaidizi Kanda ya Dar es Salaam, Idrisa Kayera (wa pili kulia) wakiwa wameshika ramani ya eneo la mradi wa viwanja 20,000.

Maeneo ambayo mradi wa viwanja 20,000 upo katika halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni unaohusisha viwanja 15,000 vilivypo Gezaulole, Vijibweni, Muongozo, Kibada na Kisola.

Kwa upande wake meya wa manispaa ya Kigamboni Ernest Mafimbo mbali na kuishukuru wizara kwa kuwapatia mradi huo, alitaka kuwepo kwa hati ya makubaliano  ya mradi kati ya  Wizara na Manispaa ya Kigamboni ili kuwa na ufanisi wakati wa usimamizi na kuendeleza mradi huo kwa maslahi ya wananchi wa kigamboni.
Chanzo: globalpublishers.co.tz