Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Manispaa Moro wapewa bil 185/- wapate maji

23b6767a650e33a2f0363ce4816524cb Manispaa Moro wapewa bil 185/- wapate maji

Mon, 21 Sep 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

SERIKALI ya Awamu ya Tano chini ya Uongozi wa Rais John Magufuli, imetoa zaidi ya Sh bilioni 185 ili kumaliza kero ya ukosefu wa maji katika Manispaa ya Morogoro

Hayo yamesemwa na mgombea ubunge wa Jimbo la Morogoro Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulaziz Abood katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni za CCM wilaya ya Morogoro Mjini . Mkutano huo ulifanyika Uwanja wa Shujaa Kata ya Mji Mpya.

Alisema kutokana na jinsi Serikali ya CCM inavyotekeleza Ilani na ahadi zake katika kuwahudumia Watanzania kwa tija, anawaomba wananchi wawachague wagombea wa CCM kwa ngazi zote yaani urais, ubunge na udiwani ili waendelee kuletea maendeleo.

Alisema: “Nimesimama hapa kwenu ili kuomba ridhaa tena kwa miaka mitano ijayo ili niweze kuendelea na kazi zilizobaki na kazi kubwa ambayo ninaijua ni kero kubwa katika mji wa Morogoro ni suala la maji."

Alisema: "Nashukuru maji tumeyapigania, na Mheshimiwa Rais John Magufuli aliweza kutupatia fedha zaidi ya shilingi bilioni 185... Wakati wowote mradi huu utaanza na kuna maeneo mengine miradi ya maji imeanza mfano ni Kata za Bigwa, Mkundi, Lukobe, Mindu na Kingolwira."

Alisema atasimamia miradi hiyo imakilike haraka ili kumaliza kero ya maji mjini Morogoro, kwa sababu akina mama wamechoka kuhangaika na ndoo za maji.

Alisema katika kipindi cha miaka kumi aliyokuwa mbunge wa jimbo hilo, hakuwa ‘mbunge wa maneno maneno’ na kwamba kwa juhudi na ushirikiano na Serikali ya Awamu ya Tano, Manispaa ya Morogoro imesonga mbele kimaendeleo.

Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Morogoro, Innocent Kalogeris, alisema jukumu kubwa kwa viongozi na wanachama wa chama hicho ni kuhakikisha majimbo matano ya ubunge yaliyobaki, wagombea wa CCM wanashinda kwa kishindo.

Chanzo: habarileo.co.tz