Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Manispaa Kigoma yawaliza machinga

41889 BIASHARA+PIC Manispaa Kigoma yawaliza machinga

Sat, 16 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kigoma.  Wajasiriamali zaidi ya 150 wanaofanya biashara ndogondogo pembezoni mwa barabara za Lumumba, Mwanga  na Stesheni Manispaa ya Kigoma Ujiji mkoani hapa  wamebomolewa vibanda vyao na uongozi wa halmashauri.

Zoezi hilo lililosimamiwa na maofisa na mgambo wa manispaa lilizua taharuki kutokana na kuambatana na uharibifu wa bidhaa na samani za wajasiriamali hao.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti leo Alhamisi 14, 2019 wajasiriamali hao wameilalamikia manispaa hiyo kuendesha zoezi la kuvunja vibanda vyao na kuharibu mali zao bila kuwapa taarifa.

Mjasiriamali mdogo wa eneo la Stesheni, Flora Wilfred amesema mgambo hao walifika katika maeneo yao wanayofanyia biashara na kuchukua mali zao.

Naye mjasiriamali Josephat Stephano, amesema kama kuna eneo jingine la biashara wawahamishie huko kuliko kuwavunjia vibanda vyao na kuwachukulia mali zao.

Diwani wa Kigoma Mjini Hussein Kalyango, amesema kwenye halmashauri hakuna zoezi hilo na halitambuliki kwani hana taarifa zozote.

Kalyango ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya huduma za jamii katika halmashauri hiyo, amesema akiwa mwenyekiti hakuna kikao kilichopitisha zoezi hilo.

Akizungumzia zoezi hilo mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji Mwailwa Pangani, amesema limefanyika kwa kufuata maelekezo ya kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa (RCC) kilichoketi hivi karibuni na kutoa maelekezo hayo.



Chanzo: mwananchi.co.tz