Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mangariba Simanjiro wanunuliwa mashine, kuacha ukeketaji

88504 Ngariba+pic Mangariba Simanjiro wanunuliwa mashine, kuacha ukeketaji

Sat, 14 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Simanjiro.  Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro, Zephania Chaula amesema mangariba 13 wamenunuliwa mashine ya kusaga nafaka na shirika lisilo la kiserikali la Nafgem ili kujipatia kipato na kuachana na ukeketaji wa watoto wa kike.

Chaula ameyasema hayo jana Desemba 13, 2019 wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Lengast kata ya Naisinyai kuhusu  kupiga vita ukatili wa kijinsia wa ukeketaji.

Amesema mangariba hao wa kijiji cha Irkujit kata ya Edonyongijape walipopatiwa mashine hiyo ya kusaga nafaka waliahidi kuachana na ukeketaji kwa maelezo kuwa walikuwa wakifanya hivyo kwa ajili ya kujipatia kipato.

Chaula amesema wanapaswa kuachana na tabia hiyo kwa kujishughulisha na masuala mengine ikiwa ni pamoja na ujasiriamali.

"Wengi wanafanya hivyo kwa kukosa shughuli za kuwaingizia kipato, mangariba mnapaswa kubadilika  mnaweza kuuza hata maziwa kuliko kuendelea kukeketa watoto wa kike mtafungwa jela," amesema Chaula.

Mwenyekiti wa kijiji cha Lengast, Tulilo Paulo amemhakikishia mkuu huyo wa wilaya kuwa wataendelea kutoa elimu ya kupiga vita ukeketaji kwenye mikutano ya kijiji.

Mkazi wa kijiji cha Lengast, Roza Lembris amesema wananchi wa eneo hilo wanazidi kuelimika kuhusu ukeketaji na wengi wameacha tabia hiyo.

Chanzo: mwananchi.co.tz